Ndugu zangu Wakristo kwa nini mnaikataa Biblia yenu ?
1) Biblia inakataza kula nguruwe lakini Nyie mnakula (na mnasema eti halali kula nguruwe!).
Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato, ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu. Msiile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao; hao ni najisi kwenu. (Biblia - Mambo ya Walawi 11:07-08)
2) Biblia inasema Mungu ni Mmoja tu lakini nyie mnasema Mungu ni watatu (Trinity).
"Yesu akamjibu, Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Mungu wetu ni Mungu mmoja." (Marko 12:29)
wakufahamu wewe ambaye pekee ni Mungu wa kweli,nakumfahamu Yesu Kristo ambaye umemtuma. (Yohana17:3)
3) Biblia inasema Yesu ni Mtu lakini nyie mnasema Yesu ni Mungu! .............................. ...........
Katika Injili ya (Yohana 8:40), Yesu anasema: "Lakini sasa mnatafuta kuniua mimi mtu ambaye nimewaambia iliyo
kweli, niliyoisikia kwa Mungu..."
4) Na Yesu anasema (katika Biblia) "Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake." lakini hamna mkristo anae Msujudie Bwana Mungu wake!!!
Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake. Biblia ( Luka 4:8 )
Nashangaa sana! Ndugu yangu Mgen, je nyie wakristo mnafuata mafundisho ya nani ? hata Biblia ambayo mnadai ni yenu mnaikataa!!!
Yesu anasema,
"Msidhani ya kuwa nimekuja kutengua sheria ya Musa au mafundisho ya Manabii, sikuja kutengua bali kukamilisha". (Mathayo 5:17)
Quran Tukufu inasema;
...Enyi Watu wa Kitabu! (Wayahudi na Wakristo) Hamna lenu jambo mpaka muishike Taurati na Injili na yote mlio teremshiwa kutokana na Mola wenu Mlezi. Na hakika ulio teremshiwa wewe kutokana na Mola wako Mlezi yatawazidishia wengi katika wao uasi na ukafiri. Basi usiwasikitikie watu makafiri. (Quran 5:68)
In short, Yesu ni Muislamu.
..Enyi Watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno lilio sawa baina yetu na nyinyi: Ya kwamba tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote; wala tusifanyane sisi kwa sisi kuwa miungu badala ya Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka basi semeni: Shuhudi- eni ya kwamba sisi ni Waislamu. (Quran 3:64)